RAIS wa Real Madrid, Florentino Perez
amesema kwamba klabu yake imekubaliana na Malaga dili la kuikosesha
Manchester City mchezaji wanayemtaka, Isco ambaye sasa atahamia
Bernabeu.
Isco, mwenye umri wa miaka 21, kwa muda
mrefu amekuwa akihusishwa na
kuhamia Madrid na kuwasili kwa kocha mpya,
Carlo Ancelotti, ambaye alitambulishwa kuwa mrithi wa Jose Mourinho
jana, ni mwanzo wa kukamilika kwa uhamisho wake.
Gazeti la Hispania, AS limenukuu Perez akiiambia Radio Nacional: "Kuna makubaliano baina ya klabu na mchezaji.
Anayetakiwa: Isco awali alisema anavutiwa kuhamia Real Madrid
Bingwa: Isco alikuwemo kwenye kikosi cha Hispania cha vijana chini ya miaak 21 kilichotwaa ubingwa wa Ulaya
"Atatambulishwa wiki ijayo baada ya vipimo vya afya,".
Taarifa nchini Hispania zinasema ada ya uhamisho itakuwa ni Euro Milioni 27.
Real pia inamtaka mshambuliaji wa Tottenham, Gareth Bale, huku Cristiano Ronaldo akiwa hatarini kuondoka.
No comments:
Post a Comment