Mmiliki wa Inter Massimo Moratti amezungumza na kusema kwamba kocha wa Chelsea Jose Mourinho atarudi kuifundisha klabu yake katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Mourinho
aliifundisha Inter kwa maiaka miwili baada ya kuondoka Chelsea mwaka
2007, akishinda makombe matatu nchini Italia likiwemo kombe la mabingwa
wa ulaya, na akishinda Serie A mara mbili mfululizo.
Na
Moratti amethibitisha kwamba kwenye mazungumzo yake ya simu na
Mourinho, kocha huyo ameonyesha nia ya kurudi Milan huko mbeleni.
"Niliongea na Mourinho kumpa hongera kwa kurudi Chelsea," Moratti alisema wakati akiongea na La Stampa.
"Nini ambacho aliniambia Jose? Aliniambia kwamba ndani ya kipindi cha miaka ijayo tutaonana tena wakati na Inter."
Jose Mourinho huko nyuma amekuwa akikaririwa kwamba Inter na Chelsea ndio timu ambazo zipo karibu na moyo wake.
No comments:
Post a Comment