Saturday, 20 July 2013

JACK WOLPER: NISIPOANGALIA, PRESHA ITANIUA.

STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ameeleza kuwa, tatizo alilonalo la presha ya kushuka huenda siku moja likawa chanzo cha kifo chake kwani linapomjia, huwa katika hali mbaya sana.
                                                                     Jacqueline Wolper.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Wolper alisema, tatizo hilo amekuwa nalo kwa muda mrefu na kufikia hatua ya kwenda kutibiwa nchini Afrika Kusini likapungua lakini sasa limerejea na linamkosesha amani.
“Kwa kweli hili tatizo la presha ya kushuka nililonalo ipo siku litaniondoa duniani, unajua wakati  mwingine hali hiyo ikinijia natokwa na damu nyingi puani, huoni ni tatizo kubwa hili!” alisema Wolper.

No comments:

Post a Comment