Saturday, 20 July 2013

MFANYA BIASHARA NA MMILIKI WA SHOPPING CENTRE AMWAGIWA TINDI KALI.

Wakuu,
Tetesi zilizonifikia ambazo SI NZURI (kwa tunaopenda kuona wenzetu hata tukiwa na tofauti nao) zinaashiria kama kuna kitu kisicho cha kawaida kimemkuta bwana huyu hii leo.

Vyanzo vyangu vya kuaminika vinanihabarisha kuwa bwana huyu yamemkuta ya kumkuta. Kuna mwenye kuwa na 'ukweli' au 'tetesi' zaidi?
Taarifa za awali zinadai kamwagiwa Tindikali maeneo ya Msasani City Mall muda wa saa 2.
Ni jirani na Ubalozi wa Marekani na jirani kabisa na Police Oysterbay.

Jamaa aliyefanya kitendo hicho alitoka mbio, mlinzi akamkimbiza lakini bahati mbaya akateleza na kuanguka na jamaa akawahi pikipiki na kutoweka eneo la tukio.

Said amelazwa Trauma (AMI) Hosp - Masaki Katika picha, ni eneo lilipotokea tukio la kumwagiwa Tindikali

No comments:

Post a Comment