Monday, 27 May 2013

KINANA: MNAOJIPITISHA URAIS KABLA YA WAKATI TUSILAUMIANE.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana.
NA BASHIIR NKOROMO, IRINGA
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amesisitiza kwamba Chama kitamwadhibu bila huruma mwanachama yeyote anayejipitisha-pitisha katika maeneo mbalimbali na kufanya kampeni za kuwania urais kabla ya wakati.
Kinana alisema hayo leo wakati akizungumza na Kamati ya Siasa na mkoa wa Iringa, katika kikao maalum, kilichofanyika kabla  ya kwenda mkoani Njombe ambako ameanza ziara ya siku saba mkoani humo.
Kinana alisema, katazo la wanachama kujipitisha-pitisha na kupiga kampeni za kuwania urais au nafasi yoyote kabla ya muda  halitoki midomoni mwa viongozi bali ni kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama.
"Ndugu zanguni, nawakumbusha kwamba kwa hili hatuna mzaha nalo, hivyo hakikisheni kila mmoja wenu kama kiongozi hajihusishi kwa namna yoyote kushiriki katika kutumiwa na wanachama hao wanaojipitishajiptisha", alisema Kinana na kuongeza;
"Ni lazima Chama kiwe kikali kwenye jambo hili, kwa sababu kama kitawaacha watu hawa kukiuka taratibu na kanunzi za Chama wanazidi kukifanya chama kuwa na makundi mengi ambayo yatakipeleka pabaya," alisema Kinana

Kinana alisema,  kazi walioyonayo wale wote wanaokitakia mema Chama, ni kumuunga mkono Mwenyekiti, Rais Jakaya katika kazi ya kuhakikisha CCM inakamilisha utekelezaji ilani yake ya Uchaguzi kwa kiwango kinachostahili na siyo muda kujipitisha pitisha mtu binaafsi kwa wanachama huku utekelezaji wa ilani ukisinzia.
Alisema kuwa hivi sasa kazi ya CCM ni kuhakikisha inatekeleza ilani ya uchaguzi kwa kipindi kilichobaki cha miaka miwili ya nusu kabla ya kumalizi kwa awamu ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete.
"Ni wazi kazi yatu CCM ni kuhakikisha tunatekeleza ilani ya uchaguzi kwa vitendo na si mamneno kama wanavyofanya wengine. ni kazi kubwa imefanyika chini ya uongozi wa Rais Kikwete na katika kipindi cha miaka miwili iliyobaki tumedhamiria kuifanya zaidi",
Alisema moja ya maeneo ambayo licha ya kuwepo changamoto za hapa na pele lakini yamefanikisha sana utekelezaji wa ilani ya CCM,  ni kwenye Halmashauri mbalimbali nchini ambapo watendaji walio wengi wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kasi.
"Kwa kweli CCM lazima hawa tuwapongeze maana kuna wengine kazi yao imebaki kuwashambulia huku wakijua watendaji hao hawana fursa ya kujitete mbele ya jamii. chapeni kazi nasi tupo nyuma yenu, na kila wakati tutakuwa tukitambua juhudi na kazi kubwa mnayoifanya kwa jamii," alisema Kinana.
Akizungumzia uchaguzi mdogo wa madini unaofanyika katika kata mbalimbali nchini Kinana, alisema CCM itashinda uchaguzi huo kwenye kata zote 25  kutokana na mtandao wa chama chake na imani inayoonekana kuwepo kwa wananchi juu ya CCM.

No comments:

Post a Comment