Madereva wa bodaboda licha ya biashara ya kusafirisha abiria, wamezua
tabia nyingine ya kufanya ngono na wateja wao wa kike, hasa wanafunzi
na wake za watu.
Imebainika kuwa baadhi ya madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda
wanatumia usafiri huo kuwarubuni na kuwashawishi wanafunzi wa kike wa
shule za msingi na sekondari na kufanya nao ngono.
Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumapili jijini Dar es Salaam katika
Wilaya za Temeke, Ilala na Kinondononi, umebaini kuwa wanafunzi wengi
wamejiingiza katika vitendo vya ngono baada ya kunaswa na ulaghai wa
madreva bodaboda wengi wakiwa vijana wadogo.
Madereva hao wamekuwa wakifanya ngono na wanafunzi, baada ya kuahidi
kuwasafirisha bure kwenda na kurudi kutoka shuleni, hasa kwa maeneo
ambayo hakuna usafiri wa daladala au eneo lililo mbali na kituo cha basi
wakati wa kutoka au kwenda shuleni.
Gazeti hili limebaini kwamba, baadhi ya walimu pia wamejiingiza katika
mchezo huo mchafu na kufanya ngono na vijana wadogo wanaoendesha
bodaboda.
Madereva hao wanaoonekana katika vituo vya daladala, huwafuata wanafunzi
hao wanaosumbuliwa na shida ya usafiri wakikataliwa kupanda daladala
makondakta wa daladala hasa wakati wa asubuhi na jioni.
No comments:
Post a Comment