Mmiliki wa klabu ya Nigeria iliyofungwa mabao 67-0 katika mechi muhimu ameamua rasm kuachana na timu hiyo kwa kuivunja.
Bubayaro
walifungwa na Police Machine, ambao walikuwa wanahangakia kupata nafasi
ya kupanda daraja kutoka kwenye ligi ya daraja la nne nchini Nigeria.
Wapinzani
wa Machine kwenye kupata nafasi ya kupanda Plateau United Feeder wao
walishinda mechi yao dhidi ya Akruba kwa mabao 79-0.
Mamlaka za soka nchini Nigeria zimezisimamisha klabu zote nne zilizohusika katika mechi hizo mbili.
Police
Machine walihitaji ushindi ili wawazidi Plateau United Feeder, lakini
matokeo ya mwisho yaliwapa nafasi Plateau kupanda daraja baada ya kuwa
na tofauti kubwa ya mabao.
Feeder ilifunga mabao 72 kati ya 79 ndani ya kipindi cha pili, wakati Machine walifunga mabao 61 baada ya mapumziko.
Mmiliki wa Bubayaro Shuaibu-Gara Ahmed Gombe, ambaye alikuwa Lagos
wakati timu yake ikichezwa sehemu nyingine, alisema kwamba alitoa amri
ya timu kutocheza mechi hiyo lakini amri yake ikadharuliwa na viongozi
wa timu.
"Mara tu niliposikia taarifa za matokeo niliamua kuivunja timu.
"Nimeandika ombi kwa Polisi wa hapa Bauchi kuchunguza suala hili la
asibu kwa soka la Nigeria na kuwakamata wote watakoku wawamehusika."
Pia inasemekana kwamba jaribio la polisi kuwakamata wachezaji baada ya
mchezo wa Bubayaro lilishindikana baada ya maofisa wa timu na wachezaji
kupotea mara tu baada ya filimbi ya mwisho.
Baadhi ya watu waliodhuria mechi hiyo wanasema kwamba kulikuwepo na
matukio kama maamuzi ya kutatanisha, kuongezwa kwa dakika za mchezo bila
sababu, maofisa wa timu ndio wakirudisha mipira kwa haraka baada ya
mabao kufungwa badala ya watoto waokota mipira.
Mwandishi wa habari ambaye alishuhudia mchezo kati ya Bubayaro dhidi ya
Police huku akiomba jina lake lisitajwa aliongea na BBC na kusema:
"Wakati wa kipindi cha pili, tulianza kushuhudia mabao ya ajabu ajabu
ya kujifunga, huku makipa wakicheza ovyo kabisa.
"Feeders walifunga kila mara. Maofisa wa timu wakageuka waokota mipira,
badala ya kutoa mpira ulioingia kwenye nyavu wakawa wanaingiza mipira
mingine uwanjani na mchezo ukaendelea hivyo .
"Kuna baadhi ya watu walikuwa wakiongea na simu kisha kuwataarifu
maofisa waliopo kwenye uwanja mwingine kuhusu kinachoendelea pale
uwanjani."
No comments:
Post a Comment