Leo tunasherehekea siku ya kuzaliwa ya mwigizaji
mwenzetu na rafiki yetu Mahsein Awadhi maarufu kama Dr.Cheni. Cheni ni
mmoja wa waigizaji wakongwe na waliojipatia sifa kubwa hapa nchini
katika kipindi chote hichi cha maisha yake. Katika pitapita zetu
tuliweza kupata maneno aliyoandikiwa na muigizaji Elizabeth Michel
katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Lulu ameandika…
“Daah..dnt even know whr to start!!!!okay....umekuwa ni mtu
muhimu sana katika maisha yangu...mtu mwenye kunipenda kwa dhati na
kunithamani...kila ninapokuwa najaribu kukuelezea huwa nakosa cha
kuongea na najisikia kulia tu....!!!nina uhakika sina cha kukulipa zaidi
ya kukuombea uishi maisha marefu yenye amani,afya na faraja!!!HAPPY
BIRTHDAY DADDY CHENI......♥”
Dr. Cheni amekuwa ni mtu wa karibu sana wa mwanadada Elizabeth
Michael na ni mmoja wa watu waliofanikisha kwa kiwango kikubwa kwenye
upatikanaji wa dhamani wa mwanadada huyu katika kesi inayomkabili.
Happy birthday Dr.Cheni.
No comments:
Post a Comment