Tuesday, 16 July 2013

Khloé Kardashian Hataki Kuachana na Lamar Odom Baada ya Skendo ya Usaliti na Kahaba.

Khloé na Lamar
Khloe Kardashian bado anahitaji kupata mtoto na mpenzi wake ambaye ni nyota wa NBA, Lamar Odom, licha ya skendo ya kumsaliti na kahaba iliyofanywa na mchezaji huyo wa timu ya Clipper, RadarOnline.com imeelezea kwa kina.

Juu ya skendo hiyo ya usaliti, “ni kweli ilimkwaza Khloe vibaya sana.  Sababu alikuwa anamuamini sana Lamar na alikuwa hana wasi pale alipomuaga na kutoka kwenda kwenye kijiwe cha makahaba mapema mwaka huu.
 
Licha ya hivyo, Khloe bado anahitaji kupata mtoto na jamaa huyo, anajisikia kwamba mara watakapopata mtoto, itaweza kuwafanya kurudi na kuwa karibu,” chanzo kiliieleza Radar. 

No comments:

Post a Comment