Wanafunzi zaidi ya 600 wanaosoma Chuo Kikuu Dodoma
(UDOM) ambao walimaliza elimu yao ya Sekondari katika shule za Kata
nchini, wamemuomba Mbunge wa Monduli,Edward Lowassa kugombea urais
katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Wawakilishi wa wanafunzi hao wapatao 40,juzi jioni
walimtembelea kiongozi huyo nyumbani kwake maeneo ya Area C mjini hapa
na kula naye chakula cha usiku, huku wakimueleza kuwa wapo tayari
kumpigia debe, kumchangia fedha za kuchukua fomu pamoja na kuwashawishi
vijana wenzao kwamba Lowassa ndiye kiongozi anayefaa kwa sasa.Hafla hiyo
pia illihudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wanafunzi hao.
No comments:
Post a Comment