MWIGIZAJI wa Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amewapongeza waandaaji wa Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013 kwani lilikuwa zuri kuliko matamasha mengine yaliyowahi kutokea Bongo.
Akizungumza na paparazi wetu, Jumapili iliyopita katika Uwanja wa Taifa lilipofanyika tamasha hilo, Dude alimpongeza Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo kwa ubunifu wake kwani tamasha hilo limefanikiwa kuwaweka watu pamoja na kuwafanya wasahau tofauti zao za kidini, kivyama na kikabila.
No comments:
Post a Comment