Tuesday, 16 July 2013

DUDE wa bongo movies apewa "shavu" la kuwa video boy wa nyimbo ya YAHAYA ya JIDE.


Mwigizaji maarufu wa bongo movies, Kulwa kikumba, maarufu kama dude amepewa nafasi ya kuwa "video boy" ama muhusika mkuu katika video mpya ya mwanadada lady jay dee YAHAYA inayotarajiwa kutoka hivi karibuni.

Katika picha mbalimbali zilizotolewa na Jay dee kupitia mtandao wa twitter na facebook zimemuonesha DUDE katika matukio mbalimbali ya ndani ya video hiyo iliyoanza kutengenezwa leo na inayotarajiwa kuachiwa ndani ya mwezi huu.
Tazama picha hizi mbalimbali za matukio ya utengenezaji huo.

No comments:

Post a Comment