Afrika kusini. Katika kazi zilizowapa
wakati mgumu washiriki wa Shindano la Big Brother The Chase basi ni kazi
ya kuoana ambayo mshiriki kutoka Tanzania Feza Kessy na mshiriki toka
Botswana Oneal wao waliamua kufunga ndoa ya kimila.
Oneal alianza kwa kuwatembelea wazazi wa Feza nyumbani kwao na kulipa posa kwa ajili ya ndoa.
Kabla ya zoezi hilo Oneal alianza kwa kumuomba Feza kwa pete ya uchumba. Binti huyo alipokubali ndipo ndoa ya kimila ikafanyika.
Akiwa ameambatana na mjomba wake Elikem na Angelo, alikuwa amevalia mavazi ya Kimasai akiwa kama mfalme wa Afrika. Dada wa Oneal alikuwa Fatima na mama yake alikuwa Natasha huku shangazi akiwa ni Annabel aliyemaliza taratibu zote za kindoa.
Mambo yote yalikwenda kama yalivyopangwa kabla baba wa bwana harusi, Sulu alipolipia mahari na wakafanya makubaliano ikiwa ni pombe na vinywaji vingine vilitumika katika kumaliza zoezi hilo.
Mama wa bwana harusi, Natasha alikuwa makini katika kumwelekeza mwanaye namna gani ya kumuongoza binti huyo katika maisha yao, huku dada wa Oneal Fatima akiendelea na kazi zingine. Pia katika jumba la Diamond Hakeem alifanya tendo hilo kwa Cleo na kumuomba kumuoa na Cleo alipokubali ndoa ikafanyika.
Wiki hii Angelo, Bimp, Cleo, Fatima, Hakeem, Nando, Pokello wapo katika kaango la kupigiwa kutolewa wiki hii. Kumpigia kura Nando unaandika neno VOTE kisha NANDO kwenda namba 15456 kupitia mitandao ya Zantel, Airtel, Vodacom na Tigo. Unaweza kumpigia kura kila baada ya saa nane na kila sms itakugharimu kiasi cha Sh600 tu.
No comments:
Post a Comment