HABARI
za wiki hii mpenzi msomaji wa safu hii. Ni matumaini yangu makubwa
kabisa kwamba umzima wa afya na unaendelea vizuri na majukumu yako ya
kimaisha bila wasiwasi wowote.
Mimi namshukuru Mungu kwa kunikutanisha nanyi kupitia safu hii. Leo nataka kuzungumzia tabia mbili ambazo mwanamke anayetaka kuingia kwenye ndoa au aliye kwenye ndoa anastahili kuwa nazo ili kuweza kumfanya ayafurahie maisha na hatimaye ndoa yake idumu mpaka mmoja wao atakapotangulia mbele za haki.
La kwanza ni mwanamke kujitahidi kuonesha kwamba, mapenzi yake kwa mwanaume husika ni ya dhati kutoka moyoni na si ya kisanii. Tujue tu kwamba, lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwanamke ili furaha ya kweli iweze kupatikana.
Sasa katika hili wapo baadhi ya wanawake wanaonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga.
Wanachotaka wao ni aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na mtu fulani ama kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume lakini sio kwamba ana mapenzi ya dhati kutoka moyoni mwake.
Mwanamke asiye na mapenzi ya dhati utamgundua tu, muda mwingi utamuona macho yake yako kwenye mfuko wa mwanaume. Akiona mfuko umetuna utaona anaonesha mapenzi ya hali ya juu lakini pindi hali inapokuwa mbaya kifedha mapenzi yanafifia.
Kwa nini wanaume wanapenda wanawake wenye mapenzi ya dhati kutoka mioyoni mwao na si kutokana na fedha walizonazo? Hii inatokana na ukweli kwamba maisha siku zote yanabadilika, kama waswahili wanavyosema, kuna kupanda na kushuka.
Siyo kwamba kila siku utakuwa na maisha mazuri na kama itatokea hivyo basi ushukuru Mungu. Hivyo basi mwanamke wa ndoa lazima afahamu hivyo na awe tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote wa maisha yao na si kwa kipindi fulani tu cha neema.
Si hivyo tu pia asilimia kubwa ya maisha ya ndoa yanatawaliwa na mapenzi, kwa hiyo nyanja hiyo inakuwa ya msingi sana kwa wanaume wengi kuiangalia ili kuepuka kuoa mwanamke ambaye baada ya muda mapenzi yanakwenda likizo.
Ndiyo maana mwanaume timamu hawezi hata siku moja kumtongoza mwanamke huku akijigamba kwa mali au fedha alizonazo. Hawezi kufanya hivyo kwa kuwa anajua kufanya hivyo ni kulazimisha kupendwa kitu ambacho madhara yake ni makubwa sana baadaye.
Lakini pia mwanamke mwenye mapenzi ya kweli kutoka moyoni ni lazima atakuwa mvumilivu kwa mwanaume. Wapo wanawake ambao siyo wavumilivu kabisa katika maisha yao.
Tunajua kwamba maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha. Huu ndiyo wakati wa kuona uvumilivu wa mtu. Kama mwanamke anatarajia kwamba siku zote ni za raha tu na pindi matatizo yanapotokea anachukua uamuzi wa kumtoroka mwanaume, huyo siyo mwanamke wa ndoa.
Wangapi leo hii huwatoroka waume zao pindi inapotokea kuumwa, kufilisika ama kupatwa na tatizo lolote ambalo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuwafanya maisha yao yakatingishika?
Uvumilivu kwa mwanamke utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati kama nilivyozungumza hapo awali. Mwanamke mwenye mapenzi ya dhati ni lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi na mumewe katika maisha ya aina yoyote, yawe ya raha ama ya starehe.

No comments:
Post a Comment