Mamlaka
ya Mawasilino Tanzania, TCRA, imesema watumiaji wa simu ambazo
hazikusajiliwa, watakatiwa mawasiliano ifikapo Juni Mosi mwaka huu.
Tamko
hilo lilitolewa jijiji Mbeya na Mkurugenzi wa Sheria na Leseni wa
mamlaka hiyo, Elizabeth Nziga wakati wa semina kuhusu utekelezaji wa
sheria mpya ya mawasiliano ya elektroniki na posta ya mwaka 2010 kwa
wadau mbalimbali.
Hiyo
ni awamu nyingine katika mipango ya TCRA, kwani awali ilikuwa na
kampeni za kuzima mitambo ya analogia nchi nzima na kuwataka wananchi
kuingia katika mfumo wa dijitali ulioanzia katika Mkoa wa Dar es Salaam
Desemba 31, mwaka jana.
Mikoa
mingine iliyoingia kwenye mfumo wa dijitali ni Arusha, Tanga, Dodoma,
Mbeya na Mwanza. Nziga alisema mamlaka hiyo inasisitiza kuwa hatua hiyo
ni utekelezaji wa makubaliano kati yake na watoa huduma za mawasilino ya
simu na kufikia usiku wa Juni Mosi, namba za simu ambazo hazikusajiliwa
zitakoma. Mmiliki wake hataweza kuitumia kupiga wala kupokea siku.