Monday, 22 July 2013

JK kuwaaga wanajeshi waliouawa.

RAIS Jakaya Kikwete leo anatarajiwa kuongoza mamia ya waombolezaji kuiaga miili ya wanajeshi saba wa Tanzania waliouawa nchini Sudan wiki iliyopita.

Wanajeshi hao walikuwa miongoni mwa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani katika Jimbo la Darfur nchini Sudan. Walivamiwa na kushambuliwa kwa risasi na waasi.

Akizungumzajana jijini Dar es Salaam kwa njia ya simu, Kaimu Msemaji wa jeshi hilo, Meja Joseph Masanja, alisema kuwa maandalizi yamekamilika na leo majira ya saa 2:30 asubuhi miili hiyo itaagwa waombolezaji wakiongozwa na Rais Kikwete pamoja na viongozi wengine wa kitaifa.

“Maandalizi yote yamekamilika. Kutakuwa na shughuli ya kuaga miili na baadaye tunasafirisha kwenda makwao kulingana na matakwa ya familia zao,” alisema.
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, aliwaongoza wananchi kuipokea miili hiyo iliyowasili juzi kwenye viwanja vya jeshi vya Air Wing, jijini Dar es Salaam.

Wanajeshi waliouawa ni Sajenti Shaibu Othuman, Koplo Oswald Chaula, Koplo Mohamed Juma, Koplo Mohamed Chikilizo, Rodney Ndunguru, Peter Werema na Fortunatus Msofe.

Kwa mujibu wa kumbukumbu za jeshi, hii ni mara ya pili kwa wanajeshi wa Tanzania kuuawa nchini humo. Awali ilikuwa Agosti mwaka jana ambapo wanajeshi watatu waliuawa.
Tanzania ina askari 850 kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani katika Jimbo la Darfur, ambao ni sehemu ya askari 1,081 wa kulinda amani katika jimbo hilo.

WEMA AJINAJISI MWEZI MTUKUFU

Stori: Shakoor Jongo na Musa Mateja
WAKATI zilipendwa wake Nasibu Abdul ‘Diamond’ akifuturisha kila kukicha, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ametupiwa madongo mazito akiambiwa amejinajisi Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kufuatia picha zake  zisizopendeza kipindi cha mfungo kutumbukizwa mtandaoni, Ijumaa Wikienda linakupa habari kamili.
 
Julai 19, mwaka huu (Chungu cha Kumi) picha za Wema ambaye ni staa wa filamu za Bongo na Miss Tanzania mwaka 2006/07 ziliingizwwa mtandaoni akiwa katika mapozi mbalimbali yenye ‘kuuchefua’ mwezi kama mtu atakumbana nazo.
 
Picha moja ilimuonesha mrembo huyo akiwa ‘klozidi’ na meneja wake, Martin Kadinda. Wanaonekana wamekumbatiana.
Picha nyingine inamuonesha Wema akipiga mbizi kwenye swimming pool moja ambayo haikufafanuliwa ni wapi nchini Tanzania.
Mbali na picha hizo mbili, nyingine ilimuonesha mlimbwende huyo akiwa katika gauni jepesi kiasi cha kuweza kuonesha ‘nido’ zake.

Sunday, 21 July 2013

MMILIKI WA INTER ASEMA BAADA YA MIAKA 3 JOSE MOURINHO ATARUDI INTER MILAN.

Mmiliki wa Inter Massimo Moratti amezungumza na kusema kwamba kocha wa Chelsea Jose Mourinho atarudi kuifundisha klabu yake katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. 

Mourinho aliifundisha Inter kwa maiaka miwili baada ya kuondoka Chelsea mwaka 2007, akishinda makombe matatu nchini Italia likiwemo kombe la mabingwa wa ulaya, na akishinda Serie A mara mbili mfululizo.

Na Moratti amethibitisha kwamba kwenye mazungumzo yake ya simu na Mourinho, kocha huyo ameonyesha nia ya kurudi Milan huko mbeleni. 


"Niliongea na Mourinho kumpa hongera kwa kurudi Chelsea," Moratti alisema wakati akiongea na La Stampa.

"Nini ambacho aliniambia Jose? Aliniambia kwamba ndani ya kipindi cha miaka ijayo tutaonana tena wakati na Inter."

Jose Mourinho huko nyuma amekuwa akikaririwa kwamba Inter na Chelsea ndio timu ambazo zipo karibu na moyo wake.

MAJANGA MUME ADUWAA MKEWE KUNASWA KWA UKAHABA

Stori:Richard Bukos
Seleman Yasin (78), mkazi wa Mtaa wa Mtamba, Msasani jijini Dar es Salaam, juzi Alhamisi aliduwaa baada ya kupata taarifa za mkewe, Saida Abdalah ‘Mama Hamisi’ (21), kunaswa kwa tuhuma za ukahaba na kupandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Jiji.
Imedaiwa mahakamani hapo kuwa Mama Hamisi alinaswa kwenye msako wa machangudoa uliofanyika usiku wa kuamkia juzi maeneo ya Buguruni.
Mume akiongea mkewe Mahakamani
Akiwa kizimbani, Mama Hamisi alisomewa shitaka la kujiuza na mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi mbele ya Hakimu Timoth Lyon.
Baada ya kusomewa shitaka lake, Mama Hamisi na makahaba wengine 13, walikana kufanya biashara hiyo kesi ikaahirishwa hadi Julai 31, mwaka huu.
Mume na mke wakiongea

Muigizaji mkongwe wa tansia ya filamu hapa Bongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ siku ya jana amefunga ndoa.

Natasha akiwa  anawekwa gauni vizuri na mpambaji wa saluni ya Partners.
Natasha akijiangalia kama yuko sawa.
…Akitengenezwa vizuri na mtaalamu wa nywele kwenye saluni hiyo.

Saturday, 20 July 2013

MFANYA BIASHARA NA MMILIKI WA SHOPPING CENTRE AMWAGIWA TINDI KALI.

Wakuu,
Tetesi zilizonifikia ambazo SI NZURI (kwa tunaopenda kuona wenzetu hata tukiwa na tofauti nao) zinaashiria kama kuna kitu kisicho cha kawaida kimemkuta bwana huyu hii leo.

Vyanzo vyangu vya kuaminika vinanihabarisha kuwa bwana huyu yamemkuta ya kumkuta. Kuna mwenye kuwa na 'ukweli' au 'tetesi' zaidi?
Taarifa za awali zinadai kamwagiwa Tindikali maeneo ya Msasani City Mall muda wa saa 2.
Ni jirani na Ubalozi wa Marekani na jirani kabisa na Police Oysterbay.

Jamaa aliyefanya kitendo hicho alitoka mbio, mlinzi akamkimbiza lakini bahati mbaya akateleza na kuanguka na jamaa akawahi pikipiki na kutoweka eneo la tukio.

Said amelazwa Trauma (AMI) Hosp - Masaki Katika picha, ni eneo lilipotokea tukio la kumwagiwa Tindikali

Serikali yazidiwa nguvu kodi ya simu.

Dar es Salaam. 
Kuna kila dalili kwamba Serikali inajipanga kufuta kodi ya Sh1,000 kila mwezi kwa wamiliki wa laini za simu baada ya kuwapo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi, taasisi na baadhi ya kampuni za simu nchini.

                                            Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa 

Hiyo inatokana na kauli ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba aliyoitoa jana akisema kwamba wizara yake ilipinga tangu awali mpango huo kabla ya kupitishwa na kuwa sheria na kwamba anaamini itaondolewa. Kauli hiyo ya Makamba imekuja siku moja baada ya chama tawala, CCM, kukaririwa na vyombo vya habari kikiitaka Serikali kuangalia vyanzo vingine vya mapato badala ya tozo hiyo.


Akizungumza kwa simu jana Makamba alisema: “Sikubaliani na hili suala na kupita kwake ilikuwa ni kuzidiwa nguvu. Lakini najua haliwezi likatekelezeka ni lazima litabadilishwa kwa kuangalia eneo lingine la kutoza kodi.”

DEMU WA PREZZO ACHANWA KWA KUTUMIA PICHA ZA UTUPU KUTAFUTA UMAARUFU!

Na Mwandishi Wetu
MDADA wa Kenya anayetajwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki Jackson Makini ‘Prezzo’, Huddah Monroe ‘The Boss Lady’ amechanwa kuwa anatumia nguvu kubwa kujipatia umaarufu kwa kupiga picha chafu kisha kuzisambaza mtandaoni.
Huddah Monroe ‘The Boss Lady’ katika pozi la utupu.
Mtandao mmoja wa nchini humo umeeleza kuwa, kuna watu wengi akiwemo Huddah ambao badala ya kufanya mambo yenye faida kwa jamii na hatimaye kuwa maarufu, wao hutumia njia batili ikiwemo hiyo ya kupiga picha za utupu.
 
Huddah katika pozi nyinine tata.
“Miaka ya nyuma ili mtu ajulikane zaidi kwenye jamii lazima afanye kazi nzuri lakini kipindi hiki ni tofauti. Wengi hasa wadada wanajipatia umaarufu kwa kuposti picha zao wakiwa watupu kwenye mitandao ya kijamii. Mfano Huddah na wengine kama vile Kim Kardashian wa Marekani,” uliandika mtandao huo.
Huddah akiwa na Prezzo.

JACK WOLPER: NISIPOANGALIA, PRESHA ITANIUA.

STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ameeleza kuwa, tatizo alilonalo la presha ya kushuka huenda siku moja likawa chanzo cha kifo chake kwani linapomjia, huwa katika hali mbaya sana.
                                                                     Jacqueline Wolper.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Wolper alisema, tatizo hilo amekuwa nalo kwa muda mrefu na kufikia hatua ya kwenda kutibiwa nchini Afrika Kusini likapungua lakini sasa limerejea na linamkosesha amani.
“Kwa kweli hili tatizo la presha ya kushuka nililonalo ipo siku litaniondoa duniani, unajua wakati  mwingine hali hiyo ikinijia natokwa na damu nyingi puani, huoni ni tatizo kubwa hili!” alisema Wolper.

Friday, 19 July 2013

SERIKALI YAPIGILIA MSUMARI KUSISITIZA TOZO LA KODI YA SIMU LIPO PALEPALE

Waziri wa Fedha, William Mgimwa, amesisitiza uamuzi wa Serikali kuendelea kutoza Sh 1,000 kwa kila mwezi kwa laini ya simu, licha ya kampuni za simu na wanasiasa kupinga.

Akizungumza na mwandishi juzi, Mgimwa alikumbusha wanaolalamikia kodi hiyo, kwamba suala la ulipaji kodi kwa taasisi au watu binafsi, ni la kisheria kulingana na mapato yao na hali halisi iliyopo.

Pia alieleza kushangazwa na matangazo ya baadhi ya kampuni kuhusu utozwaji kodi wananchi akisema wananchi ndio wanataka barabara, maji na umeme vijijini na kodi hizo zinakwenda kutumika huko. 
Kwa mujibu wa Mgimwa, kodi ya laini za simu na ya intaneti, imetengwa ikatumike kusaidia maji na uwezo wa Serikali kupeleka elimu vijijini jambo ambalo ni la maendeleo.
"Wananchi wenyewe wanalalamikia ukosefu wa huduma na baada ya Serikali kupitia na kufanyia kazi changamoto hizo, imeridhia kodi hizo wanakuja watu wanalalamika,"alisema.
Alisisitiza kuwa ongezeko la kodi kwa huduma za intaneti, ni kwa ajili ya kuboresha mfumo wa elimu ambao unalalamikiwa mara kwa mara.

MWISHO WA DUNIA,PICHA 10 ZA UTUPU ZA MISS HUYU TANZANIA 2013 ZASAMBAA,NI MTOTO WA SHEKHE.

 Mshiriki Miss Utalii Taifa 2013 Fathiya Masoud maarufa kwa jina la Mrembo wa Faceboo.
 Mrembo wa Faceboo.
Hapa Mrembo wa Faceboo akiwa ameanza kuvua nguo taratibu ilikuwa kama masihala vile.

Lulu na Bond wakikabidhiwa tuzo na vyeti vya ushindi tuzo za Ziff 2013.

PICHA: Lulu na Bond wakikabidhiwa tuzo na vyeti vya ushindi tuzo za Ziff 2013
PICHA: Lulu na Bond wakikabidhiwa tuzo na vyeti vya ushindi tuzo za Ziff 2013.

Soma maneno aliyoyaandika LULU kwa Dr.cheni kusherehekea siku yake ya kuzaliwa leo.

Soma maneno aliyoyaandika LULU kwa Dr.cheni kusherehekea siku yake ya kuzaliwa leo.
Leo tunasherehekea siku ya kuzaliwa ya mwigizaji mwenzetu na rafiki yetu Mahsein Awadhi maarufu kama Dr.Cheni. Cheni ni mmoja wa waigizaji wakongwe na waliojipatia sifa kubwa hapa nchini katika kipindi chote hichi cha maisha yake. Katika pitapita zetu tuliweza kupata maneno aliyoandikiwa na muigizaji Elizabeth Michel katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Lulu ameandika…

“Daah..dnt even know whr to start!!!!okay....umekuwa ni mtu muhimu sana katika maisha yangu...mtu mwenye kunipenda kwa dhati na kunithamani...kila ninapokuwa najaribu kukuelezea huwa nakosa cha kuongea na najisikia kulia tu....!!!nina uhakika sina cha kukulipa zaidi ya kukuombea uishi maisha marefu yenye amani,afya na faraja!!!HAPPY BIRTHDAY DADDY CHENI......♥”

Dr. Cheni amekuwa ni mtu wa karibu sana wa mwanadada Elizabeth Michael na ni mmoja wa watu waliofanikisha kwa kiwango kikubwa  kwenye upatikanaji wa dhamani wa mwanadada huyu katika kesi inayomkabili.
Happy birthday Dr.Cheni.

Tuesday, 16 July 2013

Khloé Kardashian Hataki Kuachana na Lamar Odom Baada ya Skendo ya Usaliti na Kahaba.

Khloé na Lamar
Khloe Kardashian bado anahitaji kupata mtoto na mpenzi wake ambaye ni nyota wa NBA, Lamar Odom, licha ya skendo ya kumsaliti na kahaba iliyofanywa na mchezaji huyo wa timu ya Clipper, RadarOnline.com imeelezea kwa kina.

Juu ya skendo hiyo ya usaliti, “ni kweli ilimkwaza Khloe vibaya sana.  Sababu alikuwa anamuamini sana Lamar na alikuwa hana wasi pale alipomuaga na kutoka kwenda kwenye kijiwe cha makahaba mapema mwaka huu.
 
Licha ya hivyo, Khloe bado anahitaji kupata mtoto na jamaa huyo, anajisikia kwamba mara watakapopata mtoto, itaweza kuwafanya kurudi na kuwa karibu,” chanzo kiliieleza Radar. 

DUDE wa bongo movies apewa "shavu" la kuwa video boy wa nyimbo ya YAHAYA ya JIDE.


Mwigizaji maarufu wa bongo movies, Kulwa kikumba, maarufu kama dude amepewa nafasi ya kuwa "video boy" ama muhusika mkuu katika video mpya ya mwanadada lady jay dee YAHAYA inayotarajiwa kutoka hivi karibuni.

Katika picha mbalimbali zilizotolewa na Jay dee kupitia mtandao wa twitter na facebook zimemuonesha DUDE katika matukio mbalimbali ya ndani ya video hiyo iliyoanza kutengenezwa leo na inayotarajiwa kuachiwa ndani ya mwezi huu.
Tazama picha hizi mbalimbali za matukio ya utengenezaji huo.

Meya CCM akalia kuti kavu Arusha.


Arusha. 
Kitendo cha Chadema kutetea viti vyake vinne vya udiwani kwenye uchaguzi mdogo wa juzi, kimetafsiriwa kwamba ni kumfanya Meya wa Jiji la Arusha, Gaudence Lyimo kukalia kuti kavu. Kwa ushindi wake huo, Chadema kimefikisha viti 15 kwenye Baraza la Madiwani la Arusha wakati CCM kimebakiwa kuwa na viti 12 wakati TLP ina viti sita.
 
Pia Chadema kina nafasi ya kuongeza kiti zaidi kwani ina nafasi moja ya viti maalum iliyokuwa ikishikiliwa na Rehema Mohamed aliyetimuliwa mwaka 2011.

Mwenyekiti wa madiwani wa Chadema, Isaya Doita alisema jana kwamba ushindi wa juzi ni chachu katika msimamo wa chama chao kutaka uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha urudiwe akiamini kuwa alichaguliwa kimizengwe.

Doita ambaye ni Diwani wa Ngarenaro, alisema wana imani muda si mrefu Jiji la Arusha sasa litapata Meya ambaye amechaguliwa kwa misingi ya sheria.

Chadema ilitetea viti vya Kata za Themi, Kimandolu, Kaloleni na Elerai ilivyovipoteza baada ya kuwafukuza waliokuwa madiwani wake kwa kosa la kukiuka maagizo ya Kamati Kuu ya chama hicho kuhusu mwafaka wa umeya.

Ushindi huo unakihakikishia wingi wa wajumbe katika baraza hilo la madiwani hivyo kuwa na fursa kumwondoa madarakani Meya Lyimo. Doita aliahidi kuwa chama hicho kitakaa leo kutoa msimamo kuhusu suala hilo la umeya wa Arusha.

Akizungumzia suala hilo, Katibu wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda alisema Chadema kisahau suala la kuchagua meya mpya kwani uchaguzi wake ulishapita.
Chatanda, ambaye pia anaingia katika vikao vya Baraza la Madiwani la Arusha kutokana na kuwa Mbunge wa Viti Maalumu, alisema Chadema kinapaswa kufanya kazi na meya wa sasa.

“Unajua vikao hivi vinaongozwa kwa kanuni, kwa hiyo wingi wao si hoja ya kumvua meya au kulazimisha kupitisha mambo yao,” alisema

Mamia wafurika Manispaa
Wabunge wanne wa Chadema jana waliongoza mamia ya wafuasi wa chama hicho katika shamrashamra ya kuwasindikiza madiwani wanne kwenda kujitambulisha kwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha.

Hata hivyo, furaha yao ilizimwa na polisi baada ya kumuomba Mbunge Arusha Mjini, Godbless Lema kuwatawanya.

Sunday, 14 July 2013

MADEREVA WA BODABODA WAFANYA MAPENZI NA WANAFUNZI, WALIMU NA WAKE ZA WATU.


Madereva  wa  bodaboda licha ya biashara ya kusafirisha abiria, wamezua tabia nyingine ya kufanya ngono na  wateja wao wa kike, hasa wanafunzi na wake za watu.
Imebainika kuwa baadhi ya madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda wanatumia usafiri huo kuwarubuni na kuwashawishi wanafunzi wa kike wa shule za msingi na sekondari na kufanya nao ngono.
Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumapili jijini Dar es Salaam katika Wilaya za Temeke, Ilala na Kinondononi, umebaini kuwa wanafunzi wengi wamejiingiza katika vitendo vya ngono baada ya kunaswa na ulaghai wa madreva bodaboda wengi wakiwa vijana wadogo.
Madereva hao wamekuwa wakifanya ngono na wanafunzi, baada ya kuahidi kuwasafirisha bure kwenda na kurudi kutoka shuleni, hasa kwa maeneo ambayo hakuna usafiri wa daladala au eneo lililo mbali na kituo cha basi wakati wa kutoka au kwenda shuleni.
Gazeti hili limebaini kwamba, baadhi ya walimu pia wamejiingiza katika mchezo huo mchafu na kufanya ngono na vijana wadogo wanaoendesha bodaboda.
Madereva hao wanaoonekana katika vituo vya daladala, huwafuata wanafunzi hao wanaosumbuliwa na shida ya usafiri wakikataliwa kupanda daladala makondakta wa daladala hasa wakati wa asubuhi na jioni.

SPOTTED: HASHEEM THABEET NDANI YA UWANJA WA TAIFA KWENYE MECHI YA TAIFA STARS vs UGANDA.

Mtanzania anayecheza kikapu katika Ligi ya Marekani maarufu kama NBA, Hasheem Thabeet, amekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wa soka kwenye Uwanja wa Taifa,Dar.
Thabeet anayecheza katika timu ya Thunder, aliibuka na kuwasalimia mashabiki wakati Taifa Stars ikivaa Uganda nao walimshangilia kwa nguvu sana.

SUPER STAR AUNTY EZEKIEL AFUTURISHA HOME KWAKE.


  Baadhi ya  wageni walioalikwa wakijiandaa kwa ajili ya kupata futari hiyo
Aunt Ezekiel akiwa pamoja na wageni wake akifuturu
Staa wa maarufu wa filamu Jacob Steven ‘Jb’ akipata Futari…
  Baadhi ya  wageni walioalikwa wakijiandaa kwa ajili ya kupata futari hiyo
Aunt Ezekiel akiwa pamoja na wageni wake akifuturu
Staa wa maarufu wa filamu Jacob Steven ‘Jb’ akipata Futari hiyo
Baada ya futari JB na Aunt Ezekiel wakiwa katika nyuso za furaha.
Baadhi ya maanjumati aliyoandaa Aunt.
Staa maarufu wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel jana aliandaa futari na kuwakaribisha ndugu jamaa na marafiki nyumbani kwake Mwanyamala Garage ambapo wasanii wenzake kama Jacob Steven ‘Jb’ Steve Mengele na Hartman Mbilinyi walijumuika katika mualiko huo.
PICHA: IMELDA MTEMA

Thursday, 11 July 2013

DIAMOND AFICHUA KISA CHA KULALA NA UWOYA.


SIRI nje! Lile skendo la Rais wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kudaiwa kulala na mwigizaji Irene Uwoya ambaye ni mke wa ndoa wa mwanasoka wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ limevuja.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
KISA KAMILI
Huku akijua kabisa kuwa ataibua zogo kwa kuwa Uwoya ni mke wa ndoa wa mtu, kwa mara ya kwanza, Diamond ameamua kuanika kisa kilichomfanya kujiweka kwa muda kwa Uwoya.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika cha gazeti hili, kilichomfanya Diamond kufikia hatua ya kumtongoza na kutoka naye kimapenzi, ni kitendo cha Uwoya kutoa  maneno ya kumponda huku akionesha waziwazi hali ya kumchukia kila walipokutana.
 
Irene Uwoya.
UWOYA ALIKUWA HAMPENDI DIAMOND
“Unajua Irene (Uwoya) alikuwa hampendi Diamond hata siku moja na mara nyingi alikuwa kila akimuona lazima amponde. Habari hizo zilikuwa zikimfikia mwanamuziki huyo kupitia mashoga wa mwigizaji huyo ambazo ndiyo zilichochea.
“Kufuatia hali hiyo, Diamond naye kila alipofikishiwa taarifa na mashosti wa Uwoya, alikuwa akijisikia vibaya mno ndiyo maana ‘Sukari ya Warembo’ alilazimika kumvizia Uwoya kwa hali na mali ili kumfanya ampende.

SKENDO YA UPANGAJI MATOKEO NIGERIA: MMILIKI WA TIMU ILIYOFUNGWA MABAO 67 AIVUNJA TIMU YAKE

Mmiliki wa klabu ya Nigeria iliyofungwa mabao 67-0 katika mechi muhimu ameamua rasm kuachana na timu hiyo kwa kuivunja. 
Bubayaro walifungwa na Police Machine, ambao walikuwa wanahangakia kupata nafasi ya kupanda daraja kutoka kwenye ligi ya daraja la nne nchini Nigeria. 
Wapinzani wa Machine kwenye kupata nafasi ya kupanda Plateau United Feeder wao walishinda mechi yao dhidi ya Akruba kwa mabao  79-0.
Mamlaka za soka nchini Nigeria zimezisimamisha klabu zote nne zilizohusika katika mechi hizo mbili. 
Police Machine walihitaji ushindi ili wawazidi Plateau United Feeder, lakini matokeo ya mwisho yaliwapa nafasi Plateau kupanda daraja baada ya kuwa na tofauti kubwa ya mabao. 
Feeder ilifunga mabao 72 kati ya 79 ndani ya kipindi cha pili, wakati Machine walifunga mabao 61 baada ya mapumziko. 
Mmiliki wa Bubayaro Shuaibu-Gara Ahmed Gombe, ambaye alikuwa Lagos wakati timu yake ikichezwa sehemu nyingine, alisema kwamba alitoa amri ya timu kutocheza mechi hiyo lakini amri yake ikadharuliwa na viongozi wa timu.

MAPOKEZI YA WACHEZAJI WA MANCHESTER UNITED BANKOK THAILAND.

Mapokezi yalianzia uwanja wa ndege...anagalia wanavyowazunguka aliyetangulia ni kocha wao mpya MoyesArrival: Manchester United landed in Bangkok as they prepare to get their pre-season underway
Wachezaji wa Man united wakiwasili nchini Thailand Bangkok tayari kwa kucheza mchezo wao hapo
Flashpoint: The United squad was bombarded with cameras as they land in Bangkok
The United squad was bombarded with cameras as they land in BangkokGirls just wanna have fun: Manchester United fans welcome the players as they land in Thailand
Girls just wanna have fun: Manchester United fans welcome the players as they land in Thailand
Rio akichukua mkanda baada ya kuona mapokezi ya ukweli Thailand
Manchester United fans welcome the players as they land in Thailand
Revered: The Manchester United tour bus, with Wayne Rooney on the side, is mobbed in Bangkok
Revered: The Manchester United tour bus, with Wayne Rooney on the side, is mobbed in BangkokTribute: Moyes pays respect to the monarch at Siriraj Hospital in Bangkok ahead of United's tour
Tribute: Moyes pays respect to the monarch at Siriraj Hospital in Bangkok ahead of United's tour
Manchester United
Respect: Moyes and Ryan Giggs stand next to the image of Thai King Bhumibol Adulyadej and Queen Sirikit
Respect: Moyes and Ryan Giggs stand next to the image of Thai King Bhumibol Adulyadej and Queen Sirikit
Welcome: The United squad are greeted by passionate fans in Bangkok
Welcome: The United squad are greeted by passionate fans in Bangkok

Welcome: The Manchester United squad are greeted by passionate fans in Bangkok
Welcome: The Manchester United squad are greeted by passionate fans in Bangkok
Smile for the camera: Ferdinand will be capturing behind-the-scenes footage for the club's official website
Smile for the camera: Ferdinand will be capturing behind-the-scenes footage for the club's official website